28Mwasema, ‘Iko wapi sasa nyumba ya huyo mtu mkuu, mahema ambayo watu waovu walikaa?’
29Je, hamkuwahi kuwauliza hao wanaosafiri? Je, hamkutafakari taarifa zao:
30kwamba mtu mwovu huepushwa kutoka siku ya maafa, kwamba huokolewa kutoka siku ya ghadhabu?
31Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake? Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda?
32Hupelekwa kaburini, nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake.