2“Yasikilizeni maneno yangu kwa makini; hii na iwe faraja mnayonipa mimi.
3Nivumilieni ninapozungumza, nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki.
4“Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu? Kwa nini nisikose subira?
5Niangalieni mkastaajabu; mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu.
6Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa, nao mwili wangu unatetemeka.