8ingawa ulikuwa mtu mwenye uwezo ukimiliki nchi: mtu uliyeheshimiwa, ukiishi ndani yake.
9Umewafukuza wajane mikono mitupu na kuzivunja nguvu za yatima.
10Ndiyo sababu mitego imekuzunguka pande zote, hatari ya ghafula inakutia hofu,
11ndiyo sababu ni giza sana huwezi kuona, tena ndiyo sababu mafuriko ya maji yamekufunika.
12“Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu? Juu kuliko nyota zilizo juu sana!