12“Je, Mungu hayuko katika mbingu za juu? Juu kuliko nyota zilizo juu sana!
13Hivyo wewe wasema, ‘Mungu anajua nini?’ Je, yeye huhukumu katika giza kama hilo?
14Mawingu mazito ni pazia lake, hivyo hatuoni sisi atembeapo juu ya anga la dunia.
15Je, utaifuata njia ya zamani, ambayo watu waovu waliikanyaga?
16Waliondolewa kabla ya wakati wao, misingi yao ikachukuliwa na mafuriko.