1Ndipo Ayubu akajibu:
2“Hata leo malalamiko yangu ni chungu; mkono wake ni mzito juu yangu hata nikiugua.
3Laiti ningefahamu mahali pa kumwona; laiti ningeweza kwenda mahali akaapo!
4Ningeliweka shauri langu mbele zake, na kukijaza kinywa changu na hoja.