8Wanyama wa porini wanaotamba hawajawahi kupakanyaga, wala simba azungukaye huko.
9Mikono ya mwanadamu hushambulia miamba migumu sana, na kuiacha wazi mizizi ya milima.
10Hutoboa shimo refu la kupenya chini kwa chini kwenye miamba; macho yake huona hazina zake zote.
11Hutafuta vyanzo vya mito na kuvileta vitu vilivyofichika katika nuru.
12“Lakini hekima inaweza kupatikana wapi? Ufahamu unakaa wapi?