6wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi, nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni.
7“Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji na kuketi katika kiwanja,
8vijana waliniona wakakaa kando, nao wazee walioketi wakasimama;
9wakuu wakaacha kuzungumza na kuziba vinywa vyao kwa mikono yao;
10wenye vyeo wakanyamazishwa, nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao.