15pamoja na watawala waliokuwa na dhahabu, waliozijaza nyumba zao kwa fedha.
16Au kwa nini sikufichwa ardhini kama mtoto aliyezaliwa mfu, kama mtoto mchanga ambaye kamwe hakuuona mwanga?
17Huko waovu huacha kusumbua na huko waliochoka hupumzika.
18Wafungwa nao hufurahia utulivu wao, hawasikii tena sauti ya kukemea ya kiongozi wa watumwa.
19Wadogo na wakubwa wamo humo, na mtumwa ameachiwa huru kutoka kwa bwana wake.