1Baada ya jambo hili, Ayubu akafumbua kinywa chake na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake.
2Kisha akasema:
3“Siku ya kuzaliwa kwangu na ipotelee mbali, nao usiku ule iliposemekana, ‘Mtoto wa kiume amezaliwa!’
4Siku ile na iwe giza; Mungu juu na asiiangalie; nayo nuru isiiangazie.