8Wao ni watoto wa wapumbavu wenye asili ya ubaya, waliofukuzwa watoke katika nchi.
9“Nao sasa wana wao wananidhihaki katika nyimbo; nimekuwa kitu cha dhihaka kwao.
10Wananichukia sana na kujitenga nami, wala hawasiti kunitemea mate usoni.
11Sasa kwa kuwa Mungu ameilegeza kamba ya upinde wangu na kunitesa, wamekuwa huru kunitendea waonavyo.
12Kuume kwangu kundi linashambulia; wao huitegea miguu yangu tanzi, na kunizingira.