15Vitisho vimenifunika; heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo, salama yangu imetoweka kama wingu.
16“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; siku za mateso zimenikamata.
17Usiku mifupa yangu inachoma; maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe.
18Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo; hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu.
19Yeye amenitupa kwenye matope, nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.