16“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; siku za mateso zimenikamata.
17Usiku mifupa yangu inachoma; maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe.
18Kwa uwezo wake mkuu Mungu huwa kwangu kama nguo; hushikamana nami kama ukosi wa vazi langu.
19Yeye amenitupa kwenye matope, nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20“Ee Bwana, ninakulilia wewe lakini hunijibu; ninasimama, nawe unanitazama tu.