13Huizuia njia yangu, nao hufanikiwa katika kuniletea maafa, nami sina yeyote wa kunisaidia.
14Wananijia kama watu wapitao katika ufa mpana; katikati ya magofu huja na kunishambulia.
15Vitisho vimenifunika; heshima yangu imetoweshwa kama kwa upepo, salama yangu imetoweka kama wingu.
16“Sasa maisha yangu yamefikia mwisho; siku za mateso zimenikamata.
17Usiku mifupa yangu inachoma; maumivu yanayonitafuna hayatulii kamwe.