26Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.
27Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili.
28Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada.
29Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.
30Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika; mifupa yangu inaungua kwa homa.