25Je, sikulia kwa ajili ya wale waliokuwa katika taabu? Je, nafsi yangu haikusononeka kwa ajili ya maskini?
26Lakini nilipotazamia mema, mabaya yalinijia; nilipotafuta nuru, ndipo giza lilipokuja.
27Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili.
28Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada.
29Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.