Ayubu 30

Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.

Job 30:29 (UKJV) I am a brother to dragons, and a companion to owls.

27Kusukwasukwa ndani yangu kamwe hakutulii; siku za mateso zinanikabili.

28Ninazunguka nikiwa nimeungua, lakini si kwa jua; ninasimama katika kusanyiko nikiomba msaada.

29Nimekuwa ndugu wa mbweha, rafiki wa mabundi.

30Ngozi yangu imekuwa nyeusi nayo inachunika; mifupa yangu inaungua kwa homa.

31Kinubi changu kimegeuka kuwa maombolezo, nayo filimbi yangu imekuwa sauti ya kilio.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.