12Ni moto uwakao kwa Uharibifu; ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.
13“Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu, walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu,
14nitafanya nini Mungu atakaponikabili? Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?
15Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu, si ndiye aliwaumba? Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote ndani ya mama zetu?
16“Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, au kuyaacha macho ya wajane yadhoofike,