11Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu, naam, dhambi ya kuhukumiwa.
12Ni moto uwakao kwa Uharibifu; ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.
13“Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu, walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu,
14nitafanya nini Mungu atakaponikabili? Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?
15Je, yeye aliyeniumba tumboni mwa mama yangu, si ndiye aliwaumba? Je, si ni yeye huyo mmoja aliyetuumba sote ndani ya mama zetu?