10basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine, nao wanaume wengine walale naye.
11Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu, naam, dhambi ya kuhukumiwa.
12Ni moto uwakao kwa Uharibifu; ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.
13“Kama ningewanyima haki watumishi wangu wanaume au vijakazi wangu, walipokuwa na manungʼuniko dhidi yangu,
14nitafanya nini Mungu atakaponikabili? Nitamjibu nini nitakapoitwa kutoa hesabu?