8basi wengine na wale nilichokipanda, nayo yale yote niliyootesha na yangʼolewe.
9“Kama moyo wangu umeshawishiwa na mwanamke, au kama nimevizia mlangoni mwa jirani yangu,
10basi mke wangu na asage nafaka ya mwanaume mwingine, nao wanaume wengine walale naye.
11Kwa kuwa hilo lingekuwa aibu, naam, dhambi ya kuhukumiwa.
12Ni moto uwakao kwa Uharibifu; ungekuwa umengʼoa mavuno yangu.