21na kama nimeinua mkono wangu dhidi ya yatima, nikijua kuwa nina ushawishi mahakamani,
22basi mkono wangu na unyofoke toka begani mwangu, nao na uvunjike kutoka kiungio chake.
23Kwa kuwa niliogopa uharibifu kutoka kwa Mungu, nami kwa kuuogopa utukufu wake sikuweza kufanya mambo kama hayo.
24“Kama nimeweka tumaini langu kwenye dhahabu, au kuiambia dhahabu safi, ‘Wewe ndiwe salama yangu,’
25kama nimefurahia wingi wa utajiri wangu, ustawi ambao mikono yangu ilikuwa imepata,