10Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu, naye ananiona kama adui yake.
11Ananifunga miguu kwa pingu, tena anaziangalia njia zangu zote kwa karibu.’
12“Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa, kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
13Kwa nini unamlalamikia kwamba yeye hamjibu mwanadamu?
14Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe.