28Alinikomboa nafsi yangu nisitumbukie shimoni, nami nitaishi ili kuufurahia mwanga.’
29“Mungu hufanya haya yote kwa mwanadamu; mara mbili hata mara tatu,
30ili aigeuze nafsi yake toka shimoni, ili nuru ya uzima imwangazie.
31“Ayubu, zingatia, nisikilize mimi; nyamaza, nami nitanena.
32Kama unalo lolote la kusema, unijibu; sema, kwa maana ninataka uonekane huna hatia.