3Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo.
4Roho wa Mungu ameniumba; pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.
5Unijibu basi, kama unaweza; jiandae kunikabili mimi.
6Mimi ni kama wewe mbele za Mungu; mimi pia nimetolewa kwenye udongo.
7Huna sababu ya kuniogopa, wala mkono wangu haupaswi kukulemea.