1“Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu; zingatia kila kitu nitakachosema.
2Karibu nitafungua kinywa changu; maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu.
3Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo.
4Roho wa Mungu ameniumba; pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai.
5Unijibu basi, kama unaweza; jiandae kunikabili mimi.