6Mimi ni kama wewe mbele za Mungu; mimi pia nimetolewa kwenye udongo.
7Huna sababu ya kuniogopa, wala mkono wangu haupaswi kukulemea.
8“Lakini umesema nikiwa ninakusikia, nami nilisikia maneno yenyewe:
9‘Mimi ni safi na sina dhambi; mimi ni safi na sina hatia.
10Lakini bado Mungu amepata dosari kwangu, naye ananiona kama adui yake.