4“Ningependa nikujibu wewe pamoja na marafiki zako walio pamoja nawe.
5Tazama juu mbinguni ukaone; yaangalie mawingu yaliyo juu sana juu yako.
6Je, ukitenda dhambi, inamdhuruje Mungu? Kama dhambi zako zikiwa nyingi, hilo linamfanyia nini Mungu?
7Kama wewe ni mwadilifu, unampa nini, au yeye anapokea nini mkononi kwako?
8Uovu wako unamdhuru tu mtu mwingine kama wewe, nayo haki yako inawafaa wanadamu tu.