2“Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu.
3Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu.
4Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe.
5“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake.
6Hawaachi waovu waendelee kuishi, bali huwapa walioteswa haki yao.