7Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme na kuwatukuza milele.
8Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,
9huwaonyesha yale waliyoyatenda, kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.
10Huwafanya wao kusikia maonyo, na huwaagiza kutubu uovu wao.
11Kama wakitii na kumtumikia, wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, na miaka yao katika utoshelevu.