5“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake.
6Hawaachi waovu waendelee kuishi, bali huwapa walioteswa haki yao.
7Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme na kuwatukuza milele.
8Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,
9huwaonyesha yale waliyoyatenda, kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.