19“Tuambieni yatupasayo kumwambia; hatuwezi kutayarisha shauri letu kwa sababu ya ujinga wetu.
20Je, aambiwe kwamba nataka kuongea? Je, yuko mtu ambaye angeomba kumezwa?
21Basi hakuna awezaye kulitazama jua, jinsi linavyongʼaa angani, upepo ukishafagia mawingu.
22Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu; Mungu huja katika utukufu wa kutisha.
23Yeye Mwenyezi hatuwezi kumfikia, naye ametukuzwa katika uweza; katika hukumu zake na haki yake kuu, hataonea.