9nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, na kuyafungia katika giza nene,
10nilipoamuru mipaka yake, na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,
11niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi; hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?
12“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke, au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,
13yapate kushika miisho ya dunia, na kuwakungʼuta waovu waliomo?