11niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi; hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?
12“Umepata kuiamrisha asubuhi ipambazuke, au kuyaonyesha mapambazuko mahali pake,
13yapate kushika miisho ya dunia, na kuwakungʼuta waovu waliomo?
14Dunia hubadilika kama udongo wa mfinyanzi chini ya lakiri; sura yake hukaa kama ile ya vazi.
15Waovu huzuiliwa nuru yao, nao mkono wao ulioinuliwa huvunjwa.