Ayubu 38

Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza swali, nawe unijibu.

Job 38:3 (UKJV) Gird up now your loins like a man; for I will demand of you, and answer you me.

1Kisha Bwana akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema:

2“Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa?

3Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza swali, nawe unijibu.

4“Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu.

5Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? Hakika wewe unajua! Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.