Ayubu 39

kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima, wala hakumpa fungu la akili njema.

Job 39:17 (UKJV) Because God has deprived her of wisdom, neither has he imparted to her understanding.

15bila kujali kuwa mguu waweza kuyaponda, kwamba baadhi ya wanyama wa porini wanaweza kuyakanyaga.

16Yeye huyafanyia makinda yake ukatili kama vile si yake; hajali kwamba taabu yake inaweza ikawa bure,

17kwa kuwa Mungu hakumjalia hekima, wala hakumpa fungu la akili njema.

18Lakini akunjuapo mabawa yake kukimbia, humcheka farasi pamoja na yeye aliyempanda.

19“Je, wewe humpa farasi nguvu au kuivika shingo yake manyoya marefu?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.