24Bila woga na kwa ghadhabu huimeza nchi, wala tarumbeta iliapo yeye hawezi kusimama.
25Asikiapo sauti ya baragumu yeye hulia, ‘Aha!’ Hunusa harufu ya vita toka mbali, sauti ya mtoa amri na ukelele wa vita.
26“Je, mwewe huruka kwa hekima yako na kuyakunjua mabawa yake kuelekea kusini?
27Je, tai hupaa juu kwa amri yako na kujenga kiota chake mahali pa juu?
28Huishi juu ya miamba mirefu na kukaa huko usiku; majabali yenye ncha kali ndiyo ngome yake.