1“Je, wajua ni wakati gani mbuzi wa mlimani wanapozaa? Je, watambua ni wakati gani kulungu jike azaapo mtoto wake?
2Je, waweza kuhesabu miezi hadi wazaapo? Je, unajua majira yao ya kuzaa?
3Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao; utungu wa kuzaa unakoma.
4Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani; huenda zao wala hawarudi tena.
5“Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? Ni nani aliyezifungua kamba zake?