2Je, waweza kuhesabu miezi hadi wazaapo? Je, unajua majira yao ya kuzaa?
3Wao hujiinamisha na kuzaa watoto wao; utungu wa kuzaa unakoma.
4Watoto wao hustawi na kuongezeka nguvu nyikani; huenda zao wala hawarudi tena.
5“Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? Ni nani aliyezifungua kamba zake?
6Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake, nchi ya chumvi kuwa makao yake.