5“Ni nani aliyemwachia punda-mwitu awe huru? Ni nani aliyezifungua kamba zake?
6Nimempa nchi isiyokaliwa na watu kuwa masikani yake, nchi ya chumvi kuwa makao yake.
7Huzicheka ghasia za mji, wala hasikii kelele za mwendesha gari.
8Huzunguka vilimani kwa ajili ya malisho na kutafuta kila kitu kibichi.
9“Je, nyati atakubali kukutumikia? Atakaa karibu na hori lako usiku?