9Je, una mkono kama wa Mungu, nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?
10Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari, nawe uvae heshima na enzi.
11Fungulia ukali wa ghadhabu yako, mtafute kila mwenye kiburi umshushe,
12mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo.
13Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini.