11Fungulia ukali wa ghadhabu yako, mtafute kila mwenye kiburi umshushe,
12mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo.
13Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini.
14Ndipo mimi mwenyewe nitakukubalia kuwa mkono wako mwenyewe wa kuume unaweza kukuokoa.
15“Mwangalie mnyama aitwaye Behemothi, niliyemuumba kama nilivyokuumba wewe, anayekula majani kama ngʼombe.