11Ni nani mwenye madai dhidi yangu ili nipate kumlipa? Kila kitu kilicho chini ya mbingu ni mali yangu.
12“Sitashindwa kunena juu ya maungo yake, nguvu zake na umbo lake zuri.
13Ni nani awezaye kumvua gamba lake la nje? Ni nani awezaye kumsogelea na lijamu?
14Nani athubutuye kuufungua mlango wa kinywa chake, kilichozungukwa na meno yake ya kutisha pande zote?
15Mgongo wake una safu za ngao zilizoshikamanishwa imara pamoja;