15Mgongo wake una safu za ngao zilizoshikamanishwa imara pamoja;
16kila moja iko karibu sana na mwenzake, wala hakuna hewa iwezayo kupita kati yake.
17Zimeunganishwa imara kila moja na nyingine; zimengʼangʼaniana pamoja wala haziwezi kutenganishwa.
18Akipiga chafya mwanga humetameta; macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.
19Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake; cheche za moto huruka nje.