18Akipiga chafya mwanga humetameta; macho yake ni kama mionzi ya mapambazuko.
19Mienge iwakayo humiminika kutoka kinywani mwake; cheche za moto huruka nje.
20Moshi hufuka kutoka puani mwake, kama kutoka kwenye chungu kinachotokota kwa moto wa matete.
21Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.
22Nguvu hukaa katika shingo yake; utisho hutangulia mbele yake.