21Pumzi yake huwasha makaa ya mawe, nayo miali ya moto huruka kutoka kinywani mwake.
22Nguvu hukaa katika shingo yake; utisho hutangulia mbele yake.
23Mikunjo ya nyama yake imeshikamana imara pamoja; iko imara na haiwezi kuondolewa.
24Kifua chake ni kigumu kama mwamba, kigumu kama jiwe la chini la kusagia.
25Ainukapo, mashujaa wanaogopa; hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo.