25Ainukapo, mashujaa wanaogopa; hurudi nyuma mbele yake anapokwenda kwa kishindo.
26Upanga unaomfikia haumdhuru, wala mkuki au mshale wala fumo.
27Chuma hukiona kama unyasi, na shaba kama mti uliooza.
28Mishale haimfanyi yeye akimbie; mawe ya kombeo kwake ni kama makapi.
29Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu; hucheka sauti za kugongana kwa mkuki.