26Upanga unaomfikia haumdhuru, wala mkuki au mshale wala fumo.
27Chuma hukiona kama unyasi, na shaba kama mti uliooza.
28Mishale haimfanyi yeye akimbie; mawe ya kombeo kwake ni kama makapi.
29Rungu kwake huwa kama kipande cha jani kavu; hucheka sauti za kugongana kwa mkuki.
30Sehemu zake za chini kwenye tumbo zina menomeno na mapengo kama vigae vya chungu, zikiacha mburuzo kwenye matope kama chombo chenye meno cha kupuria.