12Huipinga mipango ya wenye hila, ili mikono yao isifikie ufanisi.
13Yeye huwanasa wenye hekima katika hila yao, nayo mipango ya wadanganyifu huifagilia mbali.
14Giza huwapata wakati wa mchana; wakati wa adhuhuri hupapasa kama vile usiku.
15Humwokoa mhitaji kutokana na upanga ulioko kinywani mwao; huwaokoa kutokana na makucha ya wenye nguvu.
16Kwa hiyo maskini analo tarajio, nao udhalimu hufumba kinywa chake.