6Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo, wala udhia hauchipui kutoka ardhini.
7Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika, kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu.
8“Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, ningeliweka shauri langu mbele zake.
9Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika.
10Yeye huipa nchi mvua, huyapeleka maji kunyesha mashamba.