5Wenye njaa huyala mavuno yake, wakiyatoa hata katikati ya miiba, nao wenye kiu huitamani sana mali yake.
6Kwa maana taabu haioti kutoka kwenye udongo, wala udhia hauchipui kutoka ardhini.
7Lakini mwanadamu huzaliwa ili kutaabika, kwa hakika kama cheche za moto zirukavyo kuelekea juu.
8“Lakini ingekuwa ni mimi, ningemlalamikia Mungu, ningeliweka shauri langu mbele zake.
9Yeye hutenda maajabu yasiyoweza kutambuliwa, miujiza isiyoweza kuhesabika.